Jumanne 20 Mei 2025 - 06:35
Zakariya al-Sinwar, ndugu wa Shahidi Yahya al-Sinwar, auwawa kishahidi katika kambi ya al-Nusairat.

Hawza/ Zakariya al-Sinwar, ndugu yake Yahya al-Sinwar, ameuawa kishahidi pamoja na wanawe watatu katika shambulio lililo fanywa na utawala wa Kizayuni kwenye kambi ya al-Nusairat katikati mwa Ukanda wa Ghaza.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha  Shirika la Habari la Hawza, Zakariya al-Sinwar, ambaye alikuwa mhadhiri wa historia wa kisasa katika Chuo Kikuu cha Kiislamu, aliuliwa kishahidi pamoja na wanawe watatu katika shambulio lililo fanywa na utawala wa Kizayuni kwenye kambi ya al-Nusairat, iliyoko katikati mwa Ghaza.

Yeye alikuwa ndugu wa Yahya al-Sinwar, kamanda wa harakati ya Hamas aliyeuawa kishahidi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha